05. Hadiyth “Mnakula miti miwili ambayo siioni isipokuwa ni mibaya… “

335 – ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) aliwakhutubia watu siku ya ijumaa akasema:

ثُمّ إنّكم أيها الناس تأكلون شجرتين، لا أراهما إلاّ خَبيثَتَيْن [هذا] البصلَ والثومَ، لقد رأيتُ رسولَ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – إذا وجَدَ رِيحَهما مِن الرجلِ في المسجدِ، أمَرَ به فأُخْرِج إلى البقيعِ، فَمن أكلهما فليُمِتْهما طَبْخاً

“Enyi watu! Mnakula miti miwili ambayo siioni isipokuwa ni mibaya: kitunguu maji na kitunguu saumu. Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akihisi harufu yake kutoka kwa mtu aliyeko msikitini, basi huamrisha akatolewa na kupelekwa al-Baqiy´. Yule mwenye kuvila basi avipike.”[1]

Ameipokea Muslim, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/256)
  • Imechapishwa: 12/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy