05. Damu ya uzazi imesita kabla ya arobaini na ikazidi siku sitini

Swali 5: Wanawake wenye damu ya uzazi wanatakiwa kukaa siku arobaini ambapo haswali wala hawafungi au kinachozingatiwa ni kule kusita damu yao na pale tu itaposita basi amekwishasafika na hivyo ataanza kuswali? Ni upi muda mchache wa kusafika?

Jibu: Damu ya uzazi haina muda uliowekewak kikomo. Bali midhali anaona damu atakaa na hatoswali, hatofunga na wala mume wake hatomjamii. Akiona kusafika, hata kama ni kabla ya arobaini, haijalishi kitu kama amekaa siku kumi au siku tano peke yake, basi aswali, afunge na mume wake amjamii na hapana neno kufanya hivo.

Kilicho muhimu ni kwamba damu ya uzazi ni kitu chenye kuhisiwa na hukumu zake zimefungamana ima na kuwepo au kutokuwepo kwake. Wakati itapokuweko basi hukumu zake zitathibiti. Wakati ataposafika basi ametoka nje ya hukumu zake.

Lakini damu ya uzazi ikizidi juu ya siku sitini basi atazingatiwa ni mwenye damu ya uzazi. Hivyo atakaa muda wa zile siku zenye kuafikiana na ada ya hedhi yake tu. Baada ya hapo ataoga na kuswali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 10-11
  • Imechapishwa: 12/06/2021