05. ´Aqiydah sahihi juu ya Vitabu vya Allaah

Kuhusu kuamini vitabu vilivyoteremshwa, Allaah (Ta´ala) amemteremshia kitabu kwa kila Mtume. Amesema (Ta´ala):

لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ

“Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume Wetu kwa hoja za wazi na tukateremsha pamoja nao Kitabu na Mizani ili watu wasimamie kwa uadilifu.” (57:25)

كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗوَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

“Watu walikuwa Ummah mmoja kisha Allaah akatuma Manabii hali ya kuwa ni wabashiriaji na waonyaji na akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu kati ya watu katika waliyokhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho baada ya kuwajia hoja za wazi kwa uhusuda kati yao. Allaah akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah humwongoza amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.” (02:213)

Tunaviamini vitabu hivi, tunatambua kuwa ni vyenye kutoka kwa Allaah hali ya kuwa ni wenye kujisalimisha na maneno Yake (Ta´ala):

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ

“Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Ishaaq na Ya’quub na al-Asbaatw na aliyopewa Muusa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi kati ya mmoja yeyote miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha.” (02:136)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي أَنزَلَ مِن قَبْلُ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Enyi mlioamini! Mwaminini Allaah na Mtume Wake na Kitabu alichokiteremsha kwa Mtume Wake na Kitabu alichokiteremsha kabla. Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake na Vitabu Vyake na Mitume Yake na siku ya Mwisho, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa mbali.” (04:136)

وَقُلْ آمَنتُ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِن كِتَابٍ

“Na sema: “Nimeamini yale aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu.” (42:15)

الم ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ

Alif Laam Miym. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo kwa wenye kumcha, ambao wanaamini ghaibu na husimamisha swalah na hutoa sehemu katika vile Tulivyowaruzuku. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.” (02:01-04)

Tunaamini kuwa vitabu hivi ni katika maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) na si ya mwingine. Allaah (Ta´ala) amezungumza kwavyo kihakika kama alivyopenda na kutaka. Katika maneno haya kuna yenye kusikika kutoka Kwake nyuma ya pazia pasi na mkati na kati. Kama Allaah alivyozungumza na Muusa kihakika pasi na mkatikati. Amesema (Ta´ala):

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ

“Na alipokuja Muusa katika miadi Yetu na Mola wake akamsemesha.” (07:143)

قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي

“Akasema: “Ee Muusa hakika Mimi nimekuteua juu ya watu kwa ujumbe Wangu na maneno Yangu.” (07:144)

Maneno mengine ni yale ambayo Allaah (Ta´ala) anamsikilizisha mjumbe wa ki-Malaika na anamuamrisha amfikishie mjumbe wa kibinadamu. Amesema (Ta´ala):

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ

“Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah amsemeze isipokuwa kwa njia ya Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi au hutuma Mjumbe, kisha anamfunulia Wahy kwa idhini Yake ayatakayo. Hakika yujuu kabisa, Mwenye hekima.” (42:51)

Imani ya kuamini vitabu kunajumuisha pia kuamini zile Shari´ah zilizomo katika vitabu vyote na kwamba ilikuwa ni wajibu kwa nyumati walioteremshiwa navyo kujisalimisha navyo na kuhukumu kwa yale yaliyomo ndani. Vitabu hivi vinasadikishana na havikadhibishani. Vitabu vyote kimoja hufutwa na chenye kuteremshwa baada yake ni jambo la haki. Kwa mfano baadhi ya Shari´ah katika Tawraat zilifutwa na Injiyl. Amesema (Ta´ala) kuhusu ´Iysaa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam):

وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ

“Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu.” (03:50)

Vivyo hivyo Qur-aan ilifuta vitabu vya kimbingu vilivyotangulia. Amesema (Ta´ala):

مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ

“Kinachosadikisha yale yaliyokuja katika Vitabu vilivyokuwa kabla yake na ikividhibiti.” (05:48)

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ

“Na haikuwa vyenginevyo isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.” (68:52)

Imani ya kuamini vitabu ni jambo linalotakiwa kuwa la kijumla kwa yale yaliyotajwa kwa jumla na kwa ufafanuzi kwa yale yaliyotajwa kwa ufafanuzi.

Kuna baadhi ya majina ya vitabu ambavyo Allaah (Ta´ala) amevitaja kwa ufafanuzi. Kitabu ambacho Allaah amemteremshia Muusa kinaitwa “Tawraat”, kitabu alichoteremshiwa ´Iysaa kinaitwa “Injiyl”, kitabu alichoteremshiwa Daawuud kinaitwa “Zabuur” na kitabu alichoteremshiwa Muhammad kinaitwa “Qur-aan”. Hali kadhalika ametaja (Ta´ala) suhufi ya Ibraahiym na Muusa – Swalah na salamu ziwaendee. Tunaamini vitabu hivi kwa mujibu wa ufafanuzi uliyoelezwa.

Allaah ametaja vitabu vingi kwa njia ya ujumla bila ya kutaja kitu juu yake. Vivyo hivyo tunaviamini kwa ujumla huu. Amesema (Ta´ala):

وَقُلْ آمَنتُ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِن كِتَابٍ

“Na sema: “Nimeamini yale aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu.” (42:15)

Qur-aan Tukufu ambayo Allaah amemteremshia Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kitabu cha mwisho cha mbinguni na hakuna kitabu kingine baada yake. Kimefuta vitabu vyote vilivyotangulia na ni chenye kutumika kwa watu na majini. Amesema (Ta´ala):

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ

“Na haikuwa vyenginevyo isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.” (68:52)

Ni chenye kuenea yale mambo yote ambayo watu wanayahitajia katika dini na dunia yao. Amesema (Ta´ala):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Leo Nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu. Basi yule atakayefikwa na dharura na kushurutishwa kutokana na njaa kali pasipo kuelekea dhambi, basi hakika Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” (05:03)

Qur-aan ni miujiza na hakuna yeyote ambaye anaweza kuja na mfano wake. Amesema (Ta´ala):

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا

“Sema: “Ikiwa watajumuika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan, basi hawatoweza kuleta mfano wake, japokuwa watasaidiana wao kwa wao.” (17:88)

Kadhalika amesema (Ta´ala):

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ

“Haitokifikia ubatili mbele yake na wala nyuma yake – ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.” (41:42)

Kimehifadhiwa na kuzidishwa na kupunguzwa. Amesema (Ta´ala):

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi tumeteremsha Ukumbusho na hakika Sisi bila shaka ndio tutakaouhifadhi!” (15:09)

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mu´taqad as-Swahiyh, uk. 39-44
  • Imechapishwa: 21/06/2020