Yule anayemchinjia mtu mwingine kutokana na wasia aliyoachiwa au uwakala, basi si haramu kwake kukata chochote katika nywele, kucha wala ngozi yake kwa sababu Udhhiyah siyo ya kwake.

Yeyote anayetaka sehemu yoyote ya nywele au kucha zake mwanzoni mwa siku kumi kwa sababu hakuwa na nia ya kuchinja, kisha akawa na nia baadaye ndani ya siku hizo kumi, basi atajizuia kuanzia wakati alipoweka nia ya kuchinja.

Yeyote ambaye atahitaji kukata sehemu ya nywele au kucha zake kwa sababu anadhurika kuwa nazo – kama vile kucha kuvunjika au jeraha lenye nywele – basi hakuna ubaya. Kwani anayechinja Udhhiyah si bora zaidi kuliko Muhrim ambaye ameruhusiwa kunyoa ikiwa ni mgonjwa au ana madhara kichwani mwake. Tofauti ni kwamba Muhrim hulazimika kutoa fidia. Hata hivyo anayechinja Udhhiyah hana fidia.

Haijuzu kwa mwanamke kumwakilisha mtu achinje kwa niaba yake ili yeye aweze kukata nywele au kucha zake – kama wanavyodhani baadhi ya wanawake – kwa sababu hukumu inamhusu mwenye kuchinja mwenyewe, ni mamoja awe amemwakilisha mtu au hakufanya hivo. Ama wakili, hahusiki na katazo.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 9
  • Imechapishwa: 05/05/2025