Maamrisho yamegawanyika aina mbili.

1 – Maamrisho ya uwajibu.

2 – Maamrisho ya kupendeza.

Maamrisho ya uwajibu ni kama vile swalah. Kwa kuwa swalah ni wajibu. Maamrisho ya kupendeza ni kama kutumia Siwaak. Inapendeza.

Makatazo yamegawanyika aina mbili:

1 – Makatazo ya uharamu. Kwa mfano makatazo ya uzinzi.

2 – Makatatazo ya kuchukiza. Ni kama mfano wa makatazo ya mazungumzo baada ya swalah ya ´Ishaa.

Ni mamoja matendo hayo ni ya dhahiri, kama mfano wa swalah na swawm; au yawe yamejificha, kama mfano wa nia, kumtakasia nia Allaah, ukweli na mapenzi. Vivyo hivyo makatazo ni mamoja yawe ya dhahiri, kama mfano wa uzinzi; au yaliyojificha, kama mfano wa majivuno, kiburi, kujionyesha, vifundo, chuki na hasadi. Yote hayo yamekatazwa na hivyo mtu anatakiwa kuyaacha.

Kwa hivyo ´ibaadah imekusanya maamrisho na makatazo ya maneno na matendo, ni mamoja yenye kuonekana na yaliyojificha ambayo yametajwa na Shari´ah. Mtu akifanya aina moja wapo miongoni mwa ´ibaadah hizi akamfanyia asiyekuwa Allaah, basi ametumbukia katika shirki.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 15
  • Imechapishwa: 09/04/2023