04. Tasbiyh mara 33, Takbiyr mara 33 na Tahmiyd mara 33 wakati wa kulala

58 – ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) anasimulia jinsi ambavyo Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alivyomshtakia ugumu wa kazi za mikononi anazokutana nazo. Akamwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuomba mfanya kazi na hakumkuta. Akamwachia ujumbe ´Aaishah. Alipokuja (´alayhis-Salaam) ´Aaishah akamweleza. ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) anaelezea: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatujia na akakuta tayari tumeshapanda juu ya kitanda ambapo tukataka kusimama akasema: “Hapo hapo mlipo! Akaketi katikati yetu mpaka nikahisi ubaridi wa miguu yake kifuani mwangu. Akasema: ”Je, nisikuelezeni katika jambo bora kuliko kile mfanya kazi? Mnapoelekea kitandani kwenu au mnapokuwa tayari mpo kitandani kwenu basi semeni:

اللَّه أكْبَرُ

”Allaah ni mkubwa.”

mara 33.

سُبْـحانَ الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu”,

mara 33.

أَلْحَمْدُ لِلَّه

”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah”,

mara 33.

Hivo ni bora kwenu kuliko mtumishi.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

Semeni:

سُبْـحانَ الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu”,

mara 34.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Hii ni Dhikr wakati wa kulala. Ambaye atadumu na Dhikr hii wakati wa kulala basi hatopatwa na jambo la kuchoka. Faatwimah alimshtakia kuchoka kutokana na kazi ambapo akamwelekeza katika jambo hilo. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tumefikiwa na khabari kwamba yeyote atakayedumu na maneno haya basi hatofikwa na kuchoka kutokana na kazi na mfano wake.”[2]

[1] al-Bukhaariy (6318) na Muslim (2727).

[2] al-Kalaam at-Twayyib, uk. 28.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 68
  • Imechapishwa: 21/10/2025