04 – Sharti ya nne ya shaahadah – Kunyenyekea

Sharti ya nne ni kuyanyenyekea yale yanayofahamishwa na shahaadah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ

“Rejeeni kwa Mola wenu na jisalimisheni Kwake.”[1]

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ

“Na nani aliye bora zaidi kwa dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah ilihali ni mtendaji mema.”[2]

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ

“Anayeusalimisha uso wake kwa Allaah, naye akawa ni mfanya ihsaan, basi kwa hakika ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika.”[3]

Bi maana kwa “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”.

Maana ya kusalimisha uso wake ni kuwa ananyenyekea  na wakati huohuo ni mpwekeshaji na anafanya matendo. Yule asiyejisalimisha kwa Allaah na hafanyi matendo mema basi hakushikamana na kizingiti madhubuti. Hiyo ndio maana ya maneno Yake (´Azza wa Jall) yaliyokuja baada ya hapo:

وَمَن كَفَرَ فَلَا يَحْزُنكَ كُفْرُهُ ۚ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ فَنُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ نُمَتِّعُهُمْ قَلِيلًا ثُمَّ نَضْطَرُّهُمْ إِلَىٰ عَذَابٍ غَلِيظٍ

“Anayekufuru, basi usikuhuzunishe ukafiri wake. Kwetu ni marejeo yao, tutawajulisha yale waliyoyafanya. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani. Tunawaburudisha kidogo, kisha tutawasukumiza kwenye adhabu nzito.”[4]

Imekuja katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yawe ni yenye kufuata yale niliyokuja nayo.”

Huku ndio ukamilifu wa kujisalimisha na malengo yake.

[1] 39:54

[2] 4:125

[3] 31:22

[4] 31:23-24

  • Muhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aarij-ul-Qabuul (1/336)
  • Imechapishwa: 27/01/2025