Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake ya kwamba hakuna mwanaume anayemwita mke wake kitandani mwake ambapo akamkatalia, isipokuwa Yule ambaye yuko mbinguni anamkasirikia mpaka pale mume atapomuwia radhi.”[1]
Ameipokea Muslim.
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Malaika huhudhuria kwa yule anayetaka kukata roho na kama mtu alikuwa mwema husema: ”Toka, ee nafsi nzuri ambayo ilikuwa kwenye kiwiliwili kizuri. Toka ukiwa ni mwenye kusifiwa na pata bishara njema ya rehema, mimea yenye harufu nzuri na Mola si Mwenye kukasirika.” Kutaendelea kusemwa hivo mpaka pale inapotoka. Halafu ipandishwe juu mbinguni. Itaombewa idhini ya kuingia ambapo kutasemwa: “Ni nani huyu?” Kutasemwa kwamba ni fulani ambapo watasema: “Karibu, ee nafsi nzuri iliokuwa kwenye kiwiliwili kizuri. Toka ukiwa ni mwenye kusifiwa na pata bishara njema ya rehema, mimea yenye harufu nzuri na Mola si Mwenye kukasirika.” Hakutoacha kuendelea kusemwa hivo mpaka ifike kwenye mbingu ambayo Allaah (´Azza wa Jall) Yuko juu yake…. ”[2]
Ameipokea Imaam Ahmad katika ”al-Musnad” yake, Ibn Khuzaymah katika “Kitaab-ut-Tawhiyd” na al-Haakim katika “al-Mustadrak”.
Sa´d bin Abiy Waqqaas amesimulia:
”Wakati Sa´ad bin Mu´aadh alipohukumu juu ya Banuu Quraydhwah kwamba wauawe wale wote waliokuwa watu wazima, basi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: ”Hakika umewahukumu kwa hukumu ya Allaah aliyohukumu kwayo kutoka juu ya mbingu ya saba.”[3]
Ameipokea Ibn Sa´d, an-Nasaa´iy na al-Bayhaqiy.
Abu Hurayrah ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kutoa swadaqah yenye thamani ya sehemu ya tende moja tu kutokana na chumo halali – na hakuna kinachopanda kwa Allaah isipokuwa kilicho halali – isipokuwa hukipokea kwa mkono Wake wa kulia na humlelea mwenye nacho, mpaka kinakuwa mfano wa mlima.”[4]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah halali na wala haimstahikii Yeye kulala. Anaishusha mizani na kuinyanyua. Kwake kunapandishwa matendo ya usiku kabla ya mchana na matendo ya mchana kabla ya usiku. Pazia Yake ni Nuru; lau ataifunua, basi mwanga wa uso Wake ungeliunguza kila anachoona katika uumbaji Wake.”[5]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
[1] al-Bukhaariy (5194) na Muslim (1436). Tamko liko kwa Muslim.
[2] Ibn Maajah (4262) na Ahmad (2/364). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (3456). adh-Dhahabiy amesema:
”Ameipokea Ahmad katika ”al-Musnad” na al-Haakim katika ”al-Mustadrak” aliyesema: ”Iko kwa mujibu wa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.” (al-´Uluww, uk. 22)
[3] Ibn Sa´d katika “at-Twabaqaat al-Kubraa” (3/426), an-Nasaa’iy (8223) na al-Bayhaqiy katika “al-Asmaa’ was-Swifaat” (2/321). Swahiyh kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika ”al-´Uluww”, uk. 32, na cheni ya wapokezi ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (15).
[4] al-Bukhaariy (7430) na Muslim (702).
[5] Muslim (179).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 32-34
- Imechapishwa: 21/12/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 32-34
Imechapishwa: 21/12/2025
https://firqatunnajia.com/04-roho-inapotolewa-inapanda-mbinguni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket