Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
6 – Haangamii wala hatoweki.
7 – Wala hakuna kinachokuwa isipokuwa yale ayatakayo.
8 – Mawazo hayawezi kumfikia, fahamu haziwezi kumzunguka Yeye.
9 – Hafanani na viumbe/watu.
MAELEZO
Jumla hizi zinawaraddi Mushabbihah wanaomfananisha Muumba (Subhnaanahu wa Ta´ala) na viumbe. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]
Makusudio sio kupinga sifa za Allaah, kama wanavosema Ahl-ul-Bid´ah. Miongoni mwa maneno Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) katika ”Fiqh-ul-Akbar” ni kwamba amesema:
”Hafanani na chochote katika viumbe Wake.”
Kisha akasema (Rahimahu Allaah) baada ya hapo:
”Sifa Zake zote zinazotofautiana na sifa za viumbe. Anajua, lakini sio kama kujua kwetu. Anaweza, lakini sio kama kuweza kwetu. Anaona, lakini sio kama kuona kwetu.”
[1] 42:11
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 12-13
- Imechapishwa: 12/09/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)