Swali 04: Ni ipi hukumu ya kuwasomea Qur-aan wafu na kuweka msahafu juu ya tumbo lake[1]?

Jibu: Kuwasomea Qur-aan wafu au katika kaburi ni jambo halina msingi sahihi. Bali hilo ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Bali ni katika Bid´ah. Vivo hivyo kuweka msahafu juu ya tumbo lake ni kitu hakina msingi na ni kitu hakikuwekwa katika Shari´ah. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwekwe chuma au kitu kingine kizito juu ya tumbo lake baada ya kufa kwake ili lisivimbe.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/95).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 13
  • Imechapishwa: 10/12/2021