Swali 03: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kuhudhuria mbele ya kafiri anayetaka kukata roho na kumtamkisha shahaadah[1]?

Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kama kuna wepesi wa kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na mfanyakazi wa kiyahudi ambapo siku moja akagonjweka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaenda kumtembelea na akamtamkisha shahaadah na kumwambia:

“Sema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah`. Myahudi yule akawatazama wazazi wawili ambapo akamwambia: “Mtii Abul-Qaasim! akalitamka.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye amemwokoa kutokamana na Moto.”

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/94).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 12
  • Imechapishwa: 10/12/2021