04. Kulingana juu ya ´Arshi kumetajwa mara saba ndani ya Qur-aan

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Wanazuoni na maimamu wanasema nini kuhusu Aayah zinazozungumzia sifa ikiwa ni pamoja na maneno Yake (Ta´ala):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[2]

ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ

”Kisha akalingana juu ya mbingu iliali ni moshi, akaziambia pamoja na ardhi: ”Njooni kwa kutaka au kwa lazima. Zikasema: ”Tumekuja hali ya kuwa tumetii.”[3]?

MAELEZO

Miongoni mwa Aayah zinazozungumzia sifa ambazo kumetokea ufahamu wa kimakosa juu yake, ni suala la kulinganaa juu ya ´Arshi. Allaah ameeleza juu Yake Mwenyewe (´Azza wa Jall) kuwa amelingana juu ya ´Arshi maeneo saba ndani ya Kitabu Chake. Kila mara anasema:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.”

Kwa hivyo tukafahamu kuwa sifa hiyo ni ya kikweli, na si kama wanavosema wazushi, ya kwamba ni kutawala (استولى) juu ya ´Arshi. Wameongeza (ل) kama ambavyo mayahudi waliongeza (ن) katika Tawraat. Mayahudi walipoambiwa waseme:

حِطَّةٌ

“Tuondolee uzito wa dhambi!”[4]

Wakaongezea (ن) na kusema:

حنطة

”Ngano.”

Badala yake wanataka kula na hawataki kusamehewa. Mayahudi wamezidisha (ن) ndani ya Tawraat na hawa wengine (ل) na wakasema kuwa Ametawala (استولى) juu ya ´Arshi, na kwamba si kwamba amelingana ( اسْتَوَى) juu ya ´Arshi. Sentesi hiyo haikuthibiti katika Aayah hata moja ndani ya Qur-aan. Kwa hivyo ikafahamisha kuwa tafsiri hiyo ni batili na yenye kutupiliwa mbali.

[1] 20:05

[2] 07:54

[3] 41:11

[4] 2:58

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 27-28