25 – Ibn Miskiyn ametukhabarisha: ´Amr bin ar-Rabiy´ ametukhabarisha: Yahyaa bin Ayyuub ametukhabarisha, kutoka kwa Zahr, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Shaqiyq, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, aliyesema:
“Allaah hakuumba chochote kinachostahiki kufungwa gerezeni kwa muda mrefu kama ulimi.”
26 – Abu Bakr ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha, kutok kwa Sufyaan, kutoka kwa ´Abdullaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn ´Umar, ambaye amesema:
“Kitu chenye haki zaidi ambacho mja anatakiwa kukisafisha ni ulimi wake.”
27 – Ibn Numayr ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Idriys ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kuwa bwana mmoja amesema:
“Ee Mtume wa Allaah! Ni ipi sababu kubwa itayofanya watu kuingia Motoni?” Akasema: “vitu viwili vyenye tundu: tumbo na tupu.”[1]
28 – Abu Bakr ametukhabarisha: Hafsw bin Ghiyaath ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Awn, kutoka kwa ´Atwaa’ al-Waasitwiy, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesema:
“Mja hamchi Allah (‘Azza wa Jall) mpaka auchunge ulimi wake.”
29 – Husayn ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha: Ibn Lahiy´ah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Ayyaash bin ´Abbaas, kutoka kwa Shuyaym bin Baytaan, kutoka kwa Shufayy al-Aswbahiy, ambaye amesema:
“Anayeongea sana hukosea sana.”
30 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Usaamah ametukhabarisha, kutoka kwa Zuhayr, kutoka kwa ´Atwaa’, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:
“Jihadharini na maneno ya kubwabwaja.”
31 – ´Abdul-Wahhaab bin Najdah ametukhabarisha: ´Iysaa bin Yuunus ametukhabarisha, kutoka kwa al-Awzaa´iy, kutoka kwa Hassaan bin ´Atwiyyah, kutok kwa Shaddaad bin Aws, ambaye amesema:
“Tangu niliposilimu, sijasema neno lolote isipokuwa nalichunga na kulifunga – isipokuwa tu haya ninayoyasema hivi sasa.”
32 – Husayn bin Hasan ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha, kutoka kwa ´Umar bin Dharr, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) yuko kwenye ulimi wa kila mzungumzaji. Hivyo basi amche Allaah yule anayejua anachokisema.”[2]
33 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Rajaa’, ambaye amesimulia kwamba Luqmaan alimwambia mwanawe:
“Kama kuongea ni fedha, basi kukaa kimya ni dhahabu.”
34 – al-Huutwiy ametukhabarisha: Ibn ´Ayyaash ametukhabarisha, kutoka kwa Shurahbiyl: Nimemsikia Thawbaan, mtumwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa salllam), amesema:
“Pepo kwa yule mwenye kuudhibiti ulimi wake, akalia juu ya dhambi yake na ikamtosha nyumba yake.”[3]
[1] at-Tirmidhiy (2004). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2004).
[2] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”adh-Dhwa´iyfah” (1953).
[3] Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3929).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 10-12
- Imechapishwa: 25/06/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 10-12
Imechapishwa: 25/06/2025
https://firqatunnajia.com/04-kama-kuongea-ni-fedha-basi-kukaa-kimya-ni-dhahabu/