Wanazuoni pia wametofautiana juu mitazamo mitatu kuhusu mwenye kuvua soksi za ngozi na mfano wake baada ya kutawadha na kufuta juu yake:
1 – Kwamba wudhuu´ wake ni sahihi na hana kitu juu yake.
2 – Atapaswa kuosha miguu yake tu.
3 – Atapaswa kurudia kutawadha.
Kwa kila moja ya maono haya yamesemwa na kundi miongoni mwa Salaf. Masimulizi yao yamepokelewa na ´Abdur-Razzaaq katika ”al-Muswannaf” (1/210/809-813), Ibn Abiy Shaybah (1/187-188) na al-Bayhaqiy (1/289-290).
Hapana shaka kwamba maoni ya kwanza ndiyo yenye nguvu zaidi, kwa sababu yanaenda sambamba na kuwa kufuta ni ruhusa na kurahisishiwa kutoka kwa Allaah, ilihali kusema kinyume chake kunapingana na hayo, kama alivyosema ar-Raafi´iy punde kidogo katika suala lililotangulia. Isitoshe yanapata nguvu juu ya mitazamo hiyo miwili mingine kwa kipengele kingine, bali kwa vipengele viwili:
1 – Kwamba inawafikiana na tendo la khaliyfah mwongofu ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Imesihi kutoka kwa Abu Dhibyaan kwamba:
”Alimwona ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) akikojoa akiwa amesimama, kisha akaomba maji ambapo akatawadha, akapangusa juu ya viatu vyake, kisha akaingia msikitini akavivua viatu vyake na akaswali.”[1]
2 – Kuafikiana kwake na mtazamo sahihi, kwani lau angelipangusa juu ya kichwa chake kisha akanyoa, isingekuwa wajibu juu yake kurudia kupangusa, sembuse kurudia kutawadha. Haya ndio maoni aliyoyachagua Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah, ambaye amesema:
”Wudhuu´ wa mwenye kufuta juu ya soksi za ngozi na kilemba hauchenguki kwa kuzivua, wala kwa kumalizika muda, wala si wajibu juu yake kufuta kichwa chake wala kuosha miguu yake. Haya ndio maoni ya al-Hasan al-Baswriy. Ni kama kuondoa nywele zilizofutwa juu yake kwa mujibu wa maoni sahihi katika madhehebu ya Ahmad na maoni ya jopo la wanazuoni wengi.”[2]
Hayo pia ndio maoni ya Ibn Hazm. Rejea maneno yake na radd yake dhidi ya wale walioenda kinyume naye, hakika ni yenye thamani[3].
[1] Sharh-ul-Ma´aaniy” (1/97).
[2] al-Ikhtiyaaraat al-Fiqhiyyah, uk. 15.
[3] Tazama “al-Muhallaa” (2/105-109).
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 86-87
- Imechapishwa: 22/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 86-87
Imechapishwa: 22/04/2026
https://firqatunnajia.com/04-je-wudhuu-unachenguka-kwa-kuvua-kilichopakwa-juu-yake/