Nia haitamkwi kwa hali yoyote

Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka nia wakati wa kuswali?

Jibu: Kutamka nia ni jambo halikuwa linatambulika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakati wa Salaf. Kwa hivyo ni miongoni mwa mambo yaliyozuliwa na watu na hapana haja, kwa sababu nia mahali pake ni moyoni. Allaah ni mjuzi zaidi wa yale yaliyomo ndani ya mioyo ya waja Wake. Hutaki kusimama mbele ya asiyejua mpaka uone kuwa unatakiwa kutamka yale ninayonuia ili kumtambulisha. Hakika hapana vyengine unataka kusimama mbele ya Yule anayejua yale yanayonong´onezwa na nafsi yako, anajua heka heka zako, hali yako iliyopita na hali yako ya sasa. Kwa hivyo kutamka nia ni miongoni mwa mambo ambayo hayakuwa yakitambulika wakati wa Salaf. Isitoshe ingelikuwa ni kheri basi wangelitutangulia katika jambo hilo. Kwa hivyo haifai kwa mtu kutamka nia kwa sauti; si wakati wa kuswali wala katika ´ibaadah nyenginezo, si kimyakimya wala kwa sauti ya juu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/442)
  • Imechapishwa: 22/04/2026