Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka nia?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”[1]
Nia mahali pake ni moyoni. Haihitaji kutamkwa. Unaposimama kutawadha basi hiyo ndio nia. Hakuna mtu mwenye akili anayefanya kitendo isipokuwa amekinuia. Kwa ajili hiyo baadhi ya wanazuoni wamesema:
“Kama Allaah angetulazimisha kufanya jambo bila ya nia, basi isingeliwezekana.”
Vilevile haikupokelewa kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) kwamba walikuwa wakitamka nia. Wale mtakaowaona wanatamka nia mtaona kuwa wanafanya hivo ima kutokana na ujinga au kwa kuwafuata kichwa mchunga baadhi ya wanazuoni wenye kuonelea hivo, kwa sababu wanaona kuwa nia inatakiwa kutamkwa ili moyo ufanane na ulimi. Hata hivyo maoni yao haya si sahihi. Kama ingelikuwa kitendo hicho kimewekwa katika Shari´ah, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angeliwabainishia ummah, ima kimaneno au kimatendo.
[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/441-442)
- Imechapishwa: 22/04/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka nia?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”[1]
Nia mahali pake ni moyoni. Haihitaji kutamkwa. Unaposimama kutawadha basi hiyo ndio nia. Hakuna mtu mwenye akili anayefanya kitendo isipokuwa amekinuia. Kwa ajili hiyo baadhi ya wanazuoni wamesema:
“Kama Allaah angetulazimisha kufanya jambo bila ya nia, basi isingeliwezekana.”
Vilevile haikupokelewa kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) kwamba walikuwa wakitamka nia. Wale mtakaowaona wanatamka nia mtaona kuwa wanafanya hivo ima kutokana na ujinga au kwa kuwafuata kichwa mchunga baadhi ya wanazuoni wenye kuonelea hivo, kwa sababu wanaona kuwa nia inatakiwa kutamkwa ili moyo ufanane na ulimi. Hata hivyo maoni yao haya si sahihi. Kama ingelikuwa kitendo hicho kimewekwa katika Shari´ah, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angeliwabainishia ummah, ima kimaneno au kimatendo.
[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/441-442)
Imechapishwa: 22/04/2026
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-hukumu-ya-kutamka-nia/