04. Hadiyth “Watakuwa na mabaka na viungo vyenye kung´aa… “

178 – Zirr bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Walisema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni vipi utawatambua wale ambao hujawaona katika Ummah wako?” Akasema: “Watakuwa na mabaka na viungo vyenye kung´aa, weusiweupe, kutokana na athari ya wudhuu´.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

179- Ahmad na at-Twabaraaniy pia wamepokea Hadiyth mfano wake kutoka kwa Abu Umaamah kwa cheni ya wapokezi nzuri[2].

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/187-188)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy