04. Hadiyth “Si wema kufunga katika safari”

1056- ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisafiri na akatua mahala pamoja na Maswahabah zake. Kundi la watu wakamfanyia kibanda rafiki yao ambaye alikuwa amefunga. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampitia ambapo akasema: “Ana nini rafiki yenu? Akahisi maumivu?” Wakasema: “Hapana, ee Mtume wa Allaah, lakini amefunga.” Siku hiyo kulikuwa na upepo mkali. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Si wema kufunga katika safari.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr”.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/616)
  • Imechapishwa: 22/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy