04. Hadiyth “Mtume wa Allaah alitujilia katika msikiti wetu na mkononi mwake alikuwa na bua… “

283 – Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

أتانا رسول الله صلى الله عليه وسلم في مسجدنا، وفي يده عُرجون، فرأى في قبلة المسجد نخامةً، فأقبل عليها فحتَّها بالعرجون، ثم قال: أيُّكم يحب أن يُعرض الله عنه؟ إن أحدكم إذا قام يُصلى، فإن الله تعالى قبل وجهه، فلا يبصقن قبل  وجهه، ولا عن يمينه، وليبصق عن يساره تحت رجله اليسرى، فإن عجلت به بادرةٌ  فليتفل بثوبه هكذا، ووضعه على فيه، ثم دلكه

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitujilia katika msikiti wetu na mkononi mwake alikuwa na bua. Akaona kwenye Qiblah cha msikiti makohozi, akayaelekea na kuyakwaruza kwa bua. Kisha akasema: “Ni nani kati yenu anataka Allaah amgeuzie mgongo? Mmoja wenu anaposimama kuswali, basi hakika Allaah yuko mbele yake. Hivyo basi asiteme makohozi mbele yake wala kuliani mwake; ateme kushotoni mwake, chini ya mguu wake wa kushoto. Na kama yuko na haraka, basi ateme kwenye kitambaa chake namna hii – akakiweka mdomoni mwake – kisha baadaye akayasugua.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na wengine.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/234)
  • Imechapishwa: 15/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy