04. Hadiyth “Hakika watu wawili wenye makaburi haya wanaadhibiwa… “

160 – Abu Bakrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Wakati ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anatembea kati yangu na kati ya mtu mwengine alifika kwenye makaburi mawili akasema: “Hakika watu wawili wenye makaburi haya wanaadhibiwa. Nileteeni makuti mawili.” Mimi na yule mwenzangu tukashindana ni nani atakayeanza kuleta kuti. Nikamletea kuti na akaligawa mara mbili ambapo akaweka kuti moja kwenye kaburi moja na kuti jengine kwenye kaburi lingine. Akasema: “Pengine ikafanywa nyepesi adhabu yao muda wa kuwa [makuti hayo] bado ni kijani. Wanaadhibiwa kwa kisichokuwa kitu kikubwa; usengenyi na mkojo.”[1]

Ameipokea Ahmad, at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” ambaye tamko ni lake na Ibn Maajah kwa toleo fupi.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/177)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy