Swali: Ni ipi hukumu ya mfungaji kufanya enema kwa sababu ya haja?

Jibu: Hukumu yake ni kwamba hakuna neno kufanya hivo iwapo mgonjwa atahitajia kufanya hivo kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Hilo ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) na wanachuoni wengi ambao wanaonelea kuwa kitendo hicho hakifanani na kula na kunywa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 06
  • Imechapishwa: 29/03/2021