04. Du´aa ya kutengenezewa dini, dunia na Aakhirah

43 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

اللَّهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتِي فِيهَا مَعَاشِي، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي الَّتِي فِيهَا مَعَادِي، وَاجْعَلِ الْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْرٍ، وَاجْعَلِ الْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ

”Ee Allaah! Nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo ulinzi wa jambo langu, nitengenezee dunia yangu ambayo ndipo yalipo maisha yangu, nitengenezee Aakhirah yangu ambayo ndiyo marejeo yangu, ufanye uhai kuwa ni nyongeza kwangu katika kila kheri na kifanye kifo kuwa ni pumziko kwangu na kila shari.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ee Allaah! Nitengenezee dini yangu… “

Bi maana dini yangu ambayo ndio kifungo cha mambo yangu. Mambo ya mtu hayatengemai pasi na dini.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Nitengenezee dunia yangu… ”

Bi maana dunia ambayo ndipo anapoishi mtu. Ameanza na dini kutokana na umuhimu wake.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Nitengenezee Aakhirah yangu… ”

Bi maana mtu atafufuliwa kwenda kwa Mola Wake na kurejea Kwake kwa mara nyingine.

Du´aa hii imekusanya mema ya dunia na ya Aakhirah.

[1] Muslim (2720).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 49
  • Imechapishwa: 13/10/2025