42 – Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akiomba kwa du´aa hii:
اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي, وَجَهْلِي, وَإِسْرَافِي فِي أَمْرِي, وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي, اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي جِدِّي, وَهَزْلِي, وَخَطَئِي, وَعَمْدِي, وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي, اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ, وَمَا أَخَّرْتُ, وَمَا أَسْرَرْتُ, وَمَا أَعْلَنْتُ, وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي, أَنْتَ اَلْمُقَدِّمُ وَالْمُؤَخِّرُ, وَأَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
“Ee Allaah! Nisamehe makosa yangu, ujinga wangu, kupindukia kwangu katika amri yangu yote na yale ambayo Wewe ni mjuzi zaidi kuliko mimi. Ee Allaah! Nisamehe yale makosa yangu kwa kuteleza na ya makusudi, ya ujinga na ya mzaha – na yote hayo niko nayo. Ee Allaah! Nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, niliyoyaficha na niliyoyadhihirisha, kwani hakika Wewe ni Mwenye kutanguliza na ni Mwenye kuchelewesha; Nawe juu ya kila jambo ni Muweza.”[1]
Kuna maafikiano juu yake.
MAELEZO
Katika du´aa hii mja anatambua na kukiri madhambi yake. Aidha mtu anatambua na kukiri kumuhitaji Kwake Mola Wake. Kumwabudu Kwake ni njia moja wapo ya kukubaliwa du´aa yake. Du´aa hii ni tukufu. Muislamu anatakiwa kuiomba katika kila wakati. Ni mamoja ni ndani ya swalah na nje yake.
[1] al-Bukhaariy (6398) na Muslim (2719).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 48
- Imechapishwa: 13/10/2025
42 – Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akiomba kwa du´aa hii:
اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي, وَجَهْلِي, وَإِسْرَافِي فِي أَمْرِي, وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي, اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي جِدِّي, وَهَزْلِي, وَخَطَئِي, وَعَمْدِي, وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي, اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ, وَمَا أَخَّرْتُ, وَمَا أَسْرَرْتُ, وَمَا أَعْلَنْتُ, وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي, أَنْتَ اَلْمُقَدِّمُ وَالْمُؤَخِّرُ, وَأَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
“Ee Allaah! Nisamehe makosa yangu, ujinga wangu, kupindukia kwangu katika amri yangu yote na yale ambayo Wewe ni mjuzi zaidi kuliko mimi. Ee Allaah! Nisamehe yale makosa yangu kwa kuteleza na ya makusudi, ya ujinga na ya mzaha – na yote hayo niko nayo. Ee Allaah! Nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, niliyoyaficha na niliyoyadhihirisha, kwani hakika Wewe ni Mwenye kutanguliza na ni Mwenye kuchelewesha; Nawe juu ya kila jambo ni Muweza.”[1]
Kuna maafikiano juu yake.
MAELEZO
Katika du´aa hii mja anatambua na kukiri madhambi yake. Aidha mtu anatambua na kukiri kumuhitaji Kwake Mola Wake. Kumwabudu Kwake ni njia moja wapo ya kukubaliwa du´aa yake. Du´aa hii ni tukufu. Muislamu anatakiwa kuiomba katika kila wakati. Ni mamoja ni ndani ya swalah na nje yake.
[1] al-Bukhaariy (6398) na Muslim (2719).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 48
Imechapishwa: 13/10/2025
https://firqatunnajia.com/03-duaa-ya-kuomba-ndani-ya-swalah-na-nje-yake/