6- at-Tirmidhiy amepokea ya kwamba mtumwa wa Ibn ´Umar alimjia na kumwambia:

“Mambo yamenikuia magumu siku hizi. Nataka kuhamia Iraq.” Akasema: “Nenda Shaam, sehemu ya Mkusanyiko.”

at-Tirmidhiy amesema:

“Nzuri na geni.”

7- Yahyaa bin Sa´iyd ameeleza kutoka kwa ´Abdullaah bin Hubayrah ambaye amesema kuwa pindi Abud-Dardaa’ alikuwa ni qadhi Shaam alimwandikia Salmaan na ndani yake kulikuwa:

“Njoo katika ardhi Takatifu! Ardhi ya Jihaad!”

8- ´Alqamah amesema:

“Ka´b alikuja kwa ´Umar al-Madiynah. ´Umar akasema: “Ee Ka´b! Ni kipi kinachokuzuia kuishi al-Madiynah ambapo alihamia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akazikwa ndani yake?” Akasema: “Ee kiongozi wa waumini! Hakika mimi nimesoma katika Kitabu cha Allaah Tawraat ya kwamba Shaam ndio hazina ya Allaah katika ardhi na huko ndio kuna hazina ya Allaah kwa waja Wake.”

9- ´Atwaa’ al-Khuraasaaniy amesema:

“Pindi nilipofikiri kuhama kutoka Khuraasaan niliwaomba ushauri wanachuoni ni wapi wanapoonelea nihame na familia yangu. Wote wakasema: “Shikamana na Shaam.” Wakati nilipofika Baswrah nikawataka ushauri watu waliyoko huko ni wapi wanapoonelea nihame na familia yangu. Wote wakasema: “Shikamana na Shaam.” Nilipofika Kuufah nikawataka ushauri wanachuoni waliyoko huko ni wapi wanapoonelea nihame na familia yangu. Wote wakasema: “Shikamana na Shaam.” Pindi nilipofika Makkah nikawataka ushauri wanachuoni waliyoko huko ni wapi wanapoonelea nihame na familia yangu. Wote wakasema: “Shikamana na Shaam.” Nilipofika al-Madiynah nikawataka ushauri wanachuoni waliyoko huko ni wapi wanapoonelea nihame na familia yangu. Wote wakasema: “Shikamana na Shaam.”

Ameipokea Abu Khaythamah.

10- Wahb bin Munabbih amesema:

“Harim bin Hayyaan alisema kumwambia Uways al-Qarniy: “Ee ndugu yangu! Mimi nachelea upweke baada yako.” Uways akasema: “Sidhani kama kuna ambaye anamtambua Allaah akajihisi upweke ilihali yuko pamoja Naye.” Akasema: “Nende wapi?” Uways akaashiria kuelekea Shaam kwa mkono wake.” Akasema: “Nitajipatia riziki vipi?” Uways akasema: “Nafsi hizi zikichanganyikana na udhaifu basi hazinufaiki na kitu.”

11- Abu Bakr al-Khallaal ametaja katika kitabu chake “al-Jaamiy´” kupitia kwa Abu Bakr al-Marwaziy ambaye amesema:

“Aliulizwa Abu ´Abdillaah [Ahmad bin Hanbal]: “Unaona mtu ahame wapi endapo ataichukia ile sehemu anayoishi?” Akasema: “al-Madiynah.” Kukasemwa: “Pasipokuwa al-Madiynah?” Akasema: “Makkah.” Kukasemwa: “Pasipokuwa Makkah?” Akasema: “Shaam. Shaam ndio mahali pa Mkusanyiko.” Kisha akasema: “Dameski. Huko ndiko watakusanyika watu pindi warumi wataposhinda.”

Matamshi kama hayo yamepokelewa vilevile kwa Ishaaq bin Ibraahiym bin Haani´ na Abu Twaalib. Abu Twaalib ameweka nyongeza:

“Nikamuuliza: “Nende Dameski?” Akasema: “Ndio.” Ndipo nikasema: “Halafu Rahmah?” Akasema: “Hapana. Ni karibu na pwani.”

12- Ahmad bin Hanbal amesema:

“Mwanaume akiwa hajaoa basi aishi karibu na pwani. Hata hivyo kuna thawabu nyingi kuwa mlinzi mpakani na kuwalinda waislamu. Shaam ni ardhi iliyobarikiwa.”

13- Abu Daawuud amepokea ya kwamba Ahmad aliulizwa juu ya Hadiyth “Hakika Allaah amechukua jukumu juu yangu la kuiangalia Shaam” na mfano. Akasema:

“Ni nyingi zilizoje.”

Wakati alipoulizwa kama inahusiana na doria mpakani akasema:

“Hapana. Ardhi ya Yerusalemu iko wapi? Hadiyth inasema:

“Watu wa magharibi, Ahl-ul-Maghrib, bado wataendelea siku zote kuwa juu ya haki.”

Ni watu wa Shaam.”

14- Ya´quub bin Bukhtaan amesema:

“Nilimsikia Ahmad bin Hanbal akisema: “Nilikuwa siku zote nikiamrisha kuwabeba wanawake Shaam.” Ama sasa sifanyi hivo tena. Muda umekaribia.”

Muhannaa ameongeza kuwa amesema:

“Nachelea adui asije kushambulia kizazi changu.”

15- Hanbal amesema:

“Ahmad bin Hanbal aliulizwa ni wapi anapendelea mtu ahame na familia yake. Akajibu: “Kila mji ambapo waislamu wana ngome yenye nguvu. Kama mfano wa Dameski.”

Kwa kifupi Imaam Ahmad anapendekeza mtu aishi Shaam na ahame na wanawake na watoto katika ngome yake ilio na nguvu kama Dameski. Kuhusu sehemu za nje za Shaam na mipakani mwake karibu na pwani, hapendekezi mtu ahamie huko na familia kwa kuchelea mashambulizi ya maadui. Anapendekeza tu mtu awe huko kama mlinzi wa mpaka pasi na kwenda na familia na watoto. Kila ambavyo mtu ataishi karibu na pwani ndivyo kunakhofiwa kwake zaidi. Ndio maana amechukiza mtu kuhama huko na familia.

Kuhusu Hadiyth zinazozungumzia fadhila za Shaam, Ahmad haonelei kuwa zinahusu mipaka yake tu. Uhakika wa mambo ni kuwa ni zenye kuenea na zinahusu Shaam nzima kama Yerusalemu na maeneo yake ya jirani, Dameski na sehemu zingine na Allaah (Ta´ala) ndiye anajua zaidi.

16- Vilevile al-Awzaa´iy amechukiza mtu kuihamisha familia yake mipakani ambapo wanakhofiwa juu ya adui mbali na ile mipaka yenye usalama.

17- al-Hasan bin al-Hasan ameeleza kuwa kuna kundi la watu kutoka Yamaamah lilimjia ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz ili kutaka kuishi Dameski. Pindi alipowashauri kutofanya hivo wakamuomba awachagulie mji. Akawaambia:

“Qinnasriyiyn[1].”

Kadhalika ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz alikuwa anajichagulia juu ya nafsi yake Qinnaasriyiyn badala ya Dameski. Alichagua hivo ili awe karibu na adui. Kuwepo kwake yeye huko ni kwa ajili ya manufaa ya waislamu kwa ajili ya kuliandaa jeshi, kupata khabari kutoka kwa maadui na mambo mengine kwa ajili ya manufaa ya waislamu.

[1] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Qinnasrin

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 31-36
  • Imechapishwa: 02/02/2017