Jubayr bin Muhammad ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia bedui aliyekuwa akiomba du´aa ya kuteremshiwa mvua:

“Ole wako. Je, unajua ni nani Allaah? Hakika jambo Lake ni kuu kuliko kuombewa uombezi juu ya yeyote. Hakika Yeye yuko juu ya ‘Arshi Yake juu ya mbingu Zake.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah.

Jubayr bin Muhammad ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia bedui aliyekuwa akiomba du´aa ya kuteremshiwa mvua:

Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema katika Khutbah yake siku ya ´Arafah:

“Je, nimefikisha?” Wakasema: “Ndio.” Akawa anaashiria kidole chake mbinguni, akiwaelekezea nacho na akisema: “Ee Allaah! Shuhudia!”[2]

Ameipokea Muslim.

al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

”Tulikuwa al-Batwhaa ambapo yakapita mawingu, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Je, mnajua umbali kati ya mbingu na ardhi?” Wakasema: ”Hapana.” Akasema: “Ima ni miaka sabini na moja, sabini na mbili au sabini na tatu. Kisha kuna mbingu juu yake.” Akahesabu mbingu saba kisha akasema: ”Juu ya saba kuna bahari, baina ya chini na juu yake kina chake ni umbali kama wa mbingu hadi mbingu, kisha juu yake kuna kondoo wanane, ambao baina ya kwato zao na magoti yao ni umbali kama wa mbingu hadi mbingu, kisha juu ya migongo yao ipo ´Arshi, kisha Allaah yuko juu yake na Yeye anayajua yale mnayoyafanya.”[3]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah katika ”Kitaab-ut-Tawhiyd”. Ni nzuri kwa mujibu wa at-Tirmidhiy.

Zaynab bint Jahsh alikuwa akimwambia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ameniozesha kwako Mwingi wa rehema kutoka juu ya ‘Arshi Yake.”

Imekuja katika tamko la al-Bukhaariy:

”Hakika Allaah ameniozesha kutoka juu ya mbingu saba.”[4]

Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hivi kweli hamniamini ilihali naaminiwa na Yule aliye mbinguni? Najiwa na khabari za mbinguni asubuhi na jioni.”[5]

[1] Abu Daawuud (4726), Ibn Khuzaymah (147) na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1547). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1017), nzuri kwa mujibu wa Ibn-ul-Qayyim katika ”Mukhtaswar-us-Sawaa´iq al-Mursalah” (3/1068) na ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah.

[2] Muslim (1218).

[3] Ahmad (1/206), Abu Daawuud (4723), at-Tirmidhiy (3320), ambaye amesema kuwa ni nzuri na ngeni, Ibn Maajah (193), Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 100-102, Ibn Abiy ´Aaswim (577) na ad-Daarimiy katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 19. Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah, nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa Ibn-ul-Qayyim katika ”Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 87, na ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (577).

[4] al-Bukhaariy (7420).

[5] al-Bukhaariy (3610, 3344, 4351 na 7433), Muslim (1064) na Abu Daawuud (4764).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 30-32
  • Imechapishwa: 18/12/2025