03. Kumuomba Allaah akuongoze katika wale aliowaongoza

Kwa hivyo tunaposema katika du´aa ya Qunuut:

“Ee Allaah! Niongoze pamoja na wale Uliowaongoza.”

tunakuwa tumeomba miongozo miwili:

1 – Mwongozo wa utambuzi.

2 – Mwongozo wa matendo.

Ni kama ambavo maneno Yake Allaah (Ta´ala):

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ

“Tuongoze njia iliyonyooka.”[1]

yamekusanya miongozo miwili:

1 – Mwongozo wa utambuzi.

2 – Mwongozo wa matendo.

Kwa hivyo msomaji anatakiwa kuhudhurisha moyo kuwa anaomba miongozo miwili; mwongozo wa utambuzi na mwongozo wa matendo.

 “… pamoja na wale Uliowaongoza.”

Huku ni kufanya Tawassul kwa neema za Allaah kwa yule aliyeongozwa. Unamuomba Allaah atuneemeshe sisi pia uongofu. Maana yake ni kwamba tunakuomba uongofu, kwa sababu hivo ndivo zinavyopelekea rehema na hekima Yako. Kutokana na fadhilah Zako zilizotangulia umekwishawaongoza watu wengine.

[1] 01:06

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 07-08
  • Imechapishwa: 06/03/2024