15 – Ibn Abiy ´Umar ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Umayyah ametukhabarisha na kusema:

“’Atwaa’ alikuwa akikaa kimya kwa muda mrefu. Anapozungumza, basi tunaona kuwa anaungwa mkono.”

16 – Husayn bin Hasan ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha: Ma´mar ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

“Yeyote ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi aseme yenye kheri au anyamaze.”[1]

17 – Husayn bin Hasan ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha, kutoka kwa al-Jariyriy, kutoka kwa bwana mmoja, aliyesema:

“Nilimuona Ibn ´Abbaas amesimama kati ya Kona na Mahali pa kusimama, ameshika ncha ya ulimi wake na kusema: “Ole wako! Ongea yenye kheri utashinda. Jiepushe na shari utasalimika.” Akaambiwa: “Ee Ibn ´Abbaas, ni kwa nini unashikilia ncha ya ulimi wako?” Akasema: “Nimefikiwa na khabari kwamba hakuna kiungo chochote cha mwili kinachoweza kumdhuru zaidi mja kama ulimi wake.”

18 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Khaalid al-Ahmar ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

”´Umar aliingia kwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhumaa), ambaye alikuwa ameushika ulimi wake na kusema: “Ulimi wangu umesababisha kuangamia kwangu.”[2]

19 – ´Uthmaan bin Abî Shaybah ametukhabarisha: Abu Daawuud al-Hafariy ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Ulimi wangu huu umesababisha kuangamia kwangu.”

20 – Husayn ametukhabarisha ametukhabarisha hayohayo: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha.

21 – Husayn bin Hasan ametukhabarisha: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash, ambaye amesema:

“Wakati Shurayh alipokuwa akimsikia mtu anazungumza sana, basi husema: “Zuia matumizi yako.”

22 – Abu Muusa ametukhabarisha: ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy ametukhabarisha: Usaaamah bin Zayd ametukhabarisha, kutoka kwa baba yake Zayd bin Aslam, kutoka kwa babu yake, ambaye ameeleza:

“´Umar alikuja kwa Abu Bakr as-Swiddiyq, ambaye alikuwa ameshikilia ulimi wake na kutetemeka. Akasema: “Nini hii, ee khaliyfah wa Mtume wa Allaah?” Akasema: ”Hii imenisabanishia kuangamia kwangu.”

23 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah, Ibn Numayr na Wakiy´ wametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Yaziyd bin Hayyaan, kutoka kwa ´Anbas bin ´Uqbah, ambaye ameeleza kuwa ´Abdullaah amesema:

“Naapa kwa Yeye hapana mungu wa haki asiyekuwa Yeye! Hakuna kitu duniani kinachohitaji kufungwa gerezani kwa muda mrefu kama ulimi.”[3]

[1] al-Bukhaariy (6018) na Muslim (47).

[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (4869).

[3] Swahiyh kwa m ujibu wa a-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2858).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 8-10
  • Imechapishwa: 24/06/2025