Swali: Je, ni katika manufaa ya ulinganizi kuacha baadhi ya Sunnah kwa ajili ya kuwavuta watu?
Jibu: Ikiwa imepokelewa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyafanya yote mawili, basi hapana vibaya kuacha moja wapo. Mfano wa hilo ni kama kuswali na viatu; imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali na viatu na peku. Ukichelea kuwa watu watakimbia endapo utaswali na viatu au linasababisha fitina, basi usiswali na viatu ingawa kuswali na viatu ndio bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jitofautisheni na mayahudi wasioswali na soksi zao za ngozi wala viatu vyao.”[1]
Mfano mwingine ni kusoma kwa sauti au kimyakimya:
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
“Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”
Yote mawili yamepokelewa, ingawa sahihi zaidi ni kusoma kimyakimya kutokana na yale aliyopokea al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:
“Niliswali nyuma ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar na wote walianza swalah kwa:
الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
“Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”[2][3]
Imepokelewa pia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliisema kwa sauti ya juu[4]. Kwa hivyo matendo yote mawili yanafaa. Ukichelea matatizo endapo utaisoma kwa sauti ya juu, au kinyume chake, basi utaisoma kwa sauti ya juu, au kinyume chake. Hata hivyo usiseme:
حي على خير العمل
“Njooni katika kitendo kilicho bora.”
ili watu wasikukimbie. Usizue. Usitende dhambi. Usifanye jambo la haramu eti kwa ajili ya manufaa ya ulinganizi. Allaah (Ta´ala) ana ghera zaidi juu ya dini Yake kuliko wewe.
Vivyo hivyo kuhusu Qunuut. Endapo watakutaka uwaswalishe na usome Qunuut katika Fajr, waambie kuwa huwezi kufanya jambo hilo kwa sababu kitendo hicho hakikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth ya Anas inayosema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuacha kuendelea kuleta Qunuut mpaka alipoaga dunia.”
ni dhaifu. Imesimuliwa na Abu Ja´far ar-Raaziy ambaye kuna maoni tofauti juu yake. Maoni yenye nguvu ni kwamba ni mnyonge.
Wanapokutaka uzushe, uache jambo la wajibu au utende jambo la haramu, usifanye hivo. Wakikutaka usiseme “Aamiyn” baada ya al-Faatihah, basi waambie kuwa ima utawaswalisha na useme “Aamiyn” baada ya al-Faatihah au wasimamie wenyewe suala la kuswalisha na wewe utaswali nyuma yao – jambo ambalo linafaa.
Vivyo hivyo wakikuta usiweke mkono wako wa kulia juu ya mkono wako wa kushoto wakati unaposwali; basi unatakiwa kuwaambia kuwa utafanya hivo. Hali kadhalika kuhusiana na Sunnah nyenginezo zote ambazo hazikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa tu kwa njia moja. Usiache Sunnah kwa ajili ya kuwafurahisha watu.
[1] Abu Daawuud (652) na Ibn Hibbaan (3186). Tazama ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (659).
[2] 01:01
[3] Muslim (399).
[4] an-Nasaa’iy (904), Ibn Maajah (1788), Ibn Khuzaymah (499), ad-Daaraqutwniy (1/305) na al-Bayhaqiy (2/46).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 398-399
- Imechapishwa: 24/06/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 398-399
Imechapishwa: 24/06/2025
https://firqatunnajia.com/kuacha-sunnah-kwa-maslahi-ya-ulinganizi/