03. Hadiyth “Usiku wa safari yangu ya mbinguni niliwapitia… “

125- Mimi[1] nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Usiku wa safari yangu ya mbinguni niliwapitia watu ambao midomo yao ilikuwa ikikatwa kwa makasi ya moto. Nikasema: “Ee Jibriyl! Hawa ni watu gani?” Akajibu: “Ni wahubiri wa Ummah wako ambao wanayasema wasiyoyafanya.”[2]

[1] Bi maana Usaamah bin Zayd. Hili ni kosa kubwa na naona kuwa linatokana na kwamba mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) anategemea hifadhi yake pasi na kurejea katika msingi wake. Hadiyth ambayo amefanya hapa kuwa imesimuliwa na Usaamah bin Zayd sivyo hivyo kabisa isipokuwa imesimuliwa na Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh)  na imetolewa na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na wengineo.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/161)
  • Imechapishwa: 05/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy