Imaam ´Abdul-Ghaniy bin ´Abdil-Waahid al-Maqdisiy (Rahimahu Allaah) amesema:

196 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Nilikuwa na deni la swawm ya Ramadhaan na siwezi kuilipa isipokuwa katika Sha´baan.”[1]

Hadiyth hii inafahamisha ya kwamba hapana vibaya kuchelewa kulipa. Yule mwenye kuharakisha kulipa ndio bora zaidi. Na yule mwenye kuchelewesha hapana vibaya kwake na khaswa ikiwa kuna haja kama vile mume kumuhitajia, ugonjwa au nyudhuru nyenginezo ambazo zitapelekea yeye kuchelewesha. Wigo wa jambo hili ni mpana. Ana ruhusa ya kuchelewesha mpaka Sha´baan.

Mwenye hedhi ambaye ameacha kufunga kwa sababu ya hedhi au kwa sababu ya ugonjwa. Vilevile mwanamme akiacha kufunga kwa sababu ya maradhi au safari na hivyo akachelewesha hapana vibaya. Akiharakisha ndio bora zaidi. Haja ikipelekea kuchelewesha basi hapana vibaya kufanya hivo kutokana na Hadiyth hii. Jengine ni kwa sababu Allaah (Subhaanah) amesema:

فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“… basi atimize idadi katika masiku mengine..”[2]

Hakusema mtu aharakishe au papo hapo alipe. Bali amesema:

فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“… basi atimize idadi katika masiku mengine..”

Kwa hivyo ikafahamisha kuwa wigo wake ni mpana.

[1] al-Bukhaariy (1950) na Muslim (1146).

[2] 02:185

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ifhaam fiy Sharh ´Umdat-il-Ahkaam (01/404)
  • Imechapishwa: 17/03/2022