03. Hadiyth “Mtume wa Allaah alikuwa anapenda kushika mabua… “

283 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يعجبه العراجين أن يسمكها بيده، فدخل المسجد ذات يومٍ، وفي يده واحدٌ منها، فرأى نخاماتٍ في قبلة المسجد فحتهنَّ حتى أنقاهنَّ، ثم أقبل على الناس مغضباً فقال: أيحب أحدكم أن يستقبله رجل فيبصق في وجهه، إن أحدكم إذا قام إلى الصلاة، فإنما يستقبل ربه، والملك عن يمنيه، فلا يبصق بين يديه، ولا عن يمينه

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapenda kushika mabua kwa mkono wake. Siku moja akaingia msikitini na kwenye mkono wake mmoja alikuwa ameshika bua ambapo akaona makohozi kwenye Qiblah cha msikiti. Akayakwaruza mpaka yakaondoka kisha akawageukia watu hali ya kughadhibika akasema: “Je, anapendezwa mmoja wenu mtu asimame  mbele yake kisha akamtemea makohozi usoni mwake? Hakika mmoja wenu pindi anaposimama katika swalah, hakika anamwelekea Mola wake. Malaika yuko kuliani mwake. Hivyo basi, asiteme makohozi mbele yake wala upande wake wa kuume.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Katika tamko lingine imekuja:

فإن الله عز وجل بين أيديكم في صلاتكم، فلا توجهُوا شيئاً من الأذى بين أيديكم

“Hakika Allaah (´Azza wa Jall) yuko mbele yenu mnaposwali. Hivyo basi, msifanye chochote kisichokuwa kizuri mbele yenu.”

Ibn Khuzaymah ameiwekea kichwa cha khabari kinachosema “Makemeo ya mambo yote yasiyokuwa mazuri upande wa Qiblah wakati wa kuswali”.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/233)
  • Imechapishwa: 15/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy