02. Hadiyth “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliona makohozi kwenye Qiblah cha msikiti… “

281 – Ibn Maajah amepokea kutoka kwa al-Qaasim bin Mihraan – naye ni mtu asiyetambulika – kutoka kwa Abu Raafiy´, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema:

ن رسول الله صلى الله عليه وسلم رأى نُخَامةً في قبلة المسجد فأقبل على الناس فقال: ما بالُ أحدكم يقوم مُستقبل ربه فيخنعُ أمامه، أَيُحبُّ أحدكم أن يُستقبل فيُتَنخعَ في وجهه؟ إذا بصق أحدكم فليبصق عن شماله، أو ليتفل هكذا في ثوبه ثم أرانى إسماعيل، يعني ابن علية يبصق في ثوبه، ثم يدلكهُ

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliona makohozi kwenye Qiblah cha msikiti, ambapo akawageukia watu na kusema: “Inakuweje mmoja wenu anasimama hali ya kumuelekea Mola wake ambapo akatema makohozi mbele yake? Je, anapendezwa mmoja wenu mtu asimame  mbele yake kisha akamtemea makohozi usoni mwake? Anapotema makohozi mmoja wenu, basi ima ateme upande wa kushotoni mwake au ateme kwenye kitambaa chake.”

Ismaa´iyl – yaani Ibn ´Ulayyah – akatuonyesha namna atakavyotema kwenye kitambaa chake kisha ayasugue.[1]

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/232-233)
  • Imechapishwa: 15/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy