136- Umm-ul-Fadhwl (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kwamba usiku mmoja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Makkah akasema:
“Ee Allaah! Nimefikisha? Ee Allaah! Nimefikisha? Ee Allaah! Nimefikisha?” ´Umar bin al-Khattwaab akasimama hali ya kuangua kilio kwelikweli akasema: “Ndio. Umehamasisha, ukapambana na ukanasihi.” Ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Imani itashinda mpaka ukafiri urudi mahala pake. Bahari zitaingiliwa na Uislamu na watu watafikiwa na zama ambapo watajifunza na kuisoma Qur-aan kisha waseme: “Tumesoma na tumejua. Ni nani ambaye ni mbora kuliko sisi?” Je, kuna kheri kwa watu wale?” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni kina nani watu hao?” Akasema: “Watu hao ni miongoni mwenu. Watu hao ndio mafuta ya Moto.”[1]
Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” na cheni ya wapokezi wake ni nzuri – Allaah akitaka.
[1] Nzuri kupitia zengine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/166-167)
- Imechapishwa: 06/05/2020
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)