02. Hadiyth “Uislamu utashinda mpaka wafanya biashara… “

135- ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu utashinda mpaka wafanya biashara waanze kusafiri baharini na farasi zitumiwe katika njia ya Allaah. Kisha watajitokeza watu wanaosoma Qur-aan na kusema: “Ni nani anayesoma vyema zaidi kuliko sisi? Ni nani ambaye ni mjuzi zaidi kuliko sisi? Ni nani aliye na uelewa zaidi kuliko sisi?” Akawaambia Maswahabah zake: “Je, kuna kheri yoyote kwa watu hao?” Wakasema: “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.” Akasema: “Watu hao ni katika nyinyi, kutoka katika Ummah huu. Watu hao ndio mafuta ya Moto.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” na al-Bazzaar kwa cheni ya wapokezi isiyokuwa na neno.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/166)
  • Imechapishwa: 06/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy