385 – Ma´daan bin Abiy Twalhah amesema:

لقيتُ ثوبانَ مولى رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – فقلت: أخبِرني بعملٍ أعملُه يُدْخِلني اللهُ به الجنةَ، -أو قال: قلت: بأحبِّ الأعمالِ إلى اللهِ-. فسكتَ. ثم سألتُه، فسكتَ. ثم سألته الثالثة، فقال: سألتُ عن ذلك رسولَ اللهِ – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – فقال: عليكَ بكثرةِ السجودِ لله، فإنك لا تسجدُ لله سجدةً؛ إلا رفعكَ اللهُ بها درجةٌ، وحَطَّ بها عنكَ خطيئةً

“Nilikutana na Thawbaan, mtumwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyeachwa huru, nikasema: “Nieleze kuhusu kitendo nitachokifanya Allaah kwacho ataniingiza Peponi?” (Au nataka kujua ni kitendo kipi kinachopendeza zaidi kwa Allaah). Akanyamaza. Kisha nikamuuliza tena. Akaendelea kunyamaza. Nikamuuliza mara ya tatu, ambapo akasema: “Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya hilo. Akasema: “Hakikisha unamsujudia Allaah sana. Hakika hutomsujudia Allaah sijda, isipokuwa atakuinua ngazi na kukufutia kwayo kosa.”[1]

Ameipokea Muslim, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/277-278)
  • Imechapishwa: 23/11/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy