03. Dalili katika Sunnah kuacha swalah ni ukafiri mkubwa

Kuhusiana na Sunnah, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya mtu na shirki na kufuru ni kuacha swalah.”[1]

Ameipokea Muslim kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh).

Buraydah bin al-Huswayb (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Ahadi iliyopo baina yetu na wao ni swalah. Atakayeiacha amekufuru.”[2]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah.

Ukafiri unaokusudiwa hapa ni ule mkubwa unaomtoa mtu katika Uislamu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya swalah ndio yenye kupambanua baina ya waumini na makafiri. Ni jambo linalojulikana fika ya kwamba dini ya ukafiri sio dini ya Uislamu. Yule asiyetimiza ahadi hii basi huyo ni katika makafiri.

[1] Muslim (82).

[2] at-Tirmidhiy (2621), an-Nasaa’iy (463) na Ibn Maajah (1079). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 6-7
  • Imechapishwa: 22/10/2016