Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

3 – Hakuna chenye kumshinda.

4 – Hapana mungu wa haki asiyekuwa Yeye.

5 – Yeye ni wa kale asiyekuwa na mwanzo, wa daima asiyekuwa na mwisho.

MAELEZO

Tambua kwamba miongoni mwa majina ya Allaah sio wa Kale (القديم). Ni istilahi inayotumiwa na wanafalsafa. Kwa mujibu wa kiarabu (القديم) kunakusudiwa kitu ambacho kimetanguliwa na kingine, kwa msemo mwingine kitu cha zamani. Jina hili hutumiwa kwa kitu ambacho kimetanguliwa na kingine, na si kwa kitu ambacho hakikutanguliwa na kingine. Kama alivosema Allaah (Ta´ala):

وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ

“Mwezi Tumeukadiria vituo mpaka ukarudi mwembamba kama karara kongwe.”[1]

Bi maana mpaka kujitokeze mwezi mwandamo mwingine. Wakati kunapojitokeza mwezi mwandamo, basi huzingatiwa ule uliotangulia wa zamani (قديم), kama alivyothibitisha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah katika ”al-Majmuu´-ul-Fataawaa”[2] na Ibn Abiyl-´Izz katika maelezo yake. Hata hivyo Shaykh Ibn Maaniy´ (Rahimahu Allaah) amesema:

”Inafaa kumweleza (Subhaanah) umilele kwa njia ya maelezo. Ibn-ul-Qayyim amesema:

”Mlango wa maelezo ni mpana zaidi kuliko mlango wa sifa ambao umekomeka kwa dalili.”[3][4]

Pengine hiyo ndio sababu iliyomfanya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) wakati mwingine kutumia jina hilo.

[1] 36:39

[2] Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (1/245).

[3] Badaa’iy´-ul-Fawaa-id (1/162).

[4] Haashiyah ´alaa al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 18-21 .

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 11/09/2024