02. Vipi kuhusu funga ya mwenye hedhi aliyesafika muda mfupi kabla ya Fajr?

Swali 2: Akitwahirika mwenye hedhi na akaoga baada ya swalah ya Fajr ambapo akaswali na akakamilisha funga ya siku hiyo – je, ni lazima kuilipa siku hiyo?

Jibu: Akitwahirika mwenye hedhi kabla ya kuchomoza kwa alfajiri, japo kwa dakika moja peke yake – lakini awe na uhakika wa kusafika – basi ikiwa ni katika Ramadhaan, basi ni lazima kwake kufunga na funga ya siku hiyo inakuwa sahihi na halazimiki kuilipa. Kwa sababu amefunga akiwa msafi. Hakuna neno hata kama hatooga isipokuwa baada ya kuchomoza kwa alfajiri. Ni kama ambavo mtu akiwa na janaba inayotokamana na jimaa au kuoga ambapo akala daku na akaoga baada ya kuingia kwa alfajiri, funga yake ni sahihi.

Natumia fursa ya mnasaba huu kuzindua jambo jingine kwa wanawake. Mwanamke ikimjia hedhi na yeye amefunga siku hiyo, baadhi ya wanawake wanafikiri ikimjia hedhi yake baada ya kukata swawm kabla hajaswali ´Ishaa, basi funga ya siku hiyo inaharibika. Dhana hii haina msingi wowote. Bali akipata hedhi baada ya kuzama kwa jua, ingawa ni kwa muda mfupi tu, basi funga yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 8
  • Imechapishwa: 05/06/2021