Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mwenye fadhilah na neema, aliyeweka Shari´ah ya kufunga kwa ajili ya kuzitakasa nafsi kutokana na madhambi. Swalah na salamu zimshukie Nabii wetu Muhammad – mbora kuliko wote aliyeswali na aliyefunga, aliyeendelea juu ya kheri na akasimama sawa – na juu ya familia yake, Maswahabah wake na wote waliomfuata daima.
Ama baada ya hayo,
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah.”[1]
Aayah zilizo baada yake. Allaah (Subhaanah) ameeleza katika Aayah hizi Tukufu kwamba ameandika swawm juu ya ummah huu kama alivyoiandika juu ya ummah zilizotangulia. Kuandika hapa maana yake ni kufaradhisha. Kwa hivyo swawm imefaradhishwa juu ya ummah huu na juu ya ummah zilizokuwa kabla yake. Baadhi ya wanazuoni wamesema katika tafsiri ya Aayah hii kwamba ´ibaadah ya swawm iliandikwa juu ya Mitume na juu ya ummah zao kuanzia Aadam mpaka mwisho wa zama. Allaah ameitaja hali hii kwa sababu jambo gumu linapokuwa la pamoja kwa wote huwa ni rahisi zaidi kulikubali kwa nafsi na huzidisha utulivu wake.
Kwa hiyo swawm ni faradhi juu ya ummah zote, hata kama namna yake na wakati wake vilitofautiana. Sa´iyd bin Jubayr amesema:
”Swawm ya waliotutangulia ilikuwa kuanzia baada ya ´Ishaa mpaka usiku unaofuata, kama ilivyokuwa mwanzoni mwa Uislamu.”
Hasan amesema:
”Swawm ya Ramadhaan ilikuwa ni wajibu juu ya mayahudi, lakini wakaiacha na wakafunga siku moja katika mwaka wakidai kuwa ni siku aliyozama Fir´awn, ingawa wamedanganya katika hilo, kwani siku hiyo ni ´Aashuuraa. Swawm pia ilikuwa wajibu juu ya manaswara, lakini baada ya kufunga kwa muda mrefu walikumbana na joto kali ambapo ikawa ni jambo gumu kwao katika safari na maisha yao. Basi wanazuoni wao na viongozi wao wakakubaliana kuiweka swawm yao katika majira kati ya baridi na joto, wakaifanya iwe katika masika na wakaigeuza iwe katika wakati usiobadilika. Kisha wakasema wakati wa kuibadilisha kwamba waongeze siku kumi kama kafara kwa tulichofanya ambapo kwa jumla yake siku arobaini.”
[1] 02:183
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 11-12
- Imechapishwa: 25/01/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 11-12
Imechapishwa: 25/01/2026
https://firqatunnajia.com/02-ni-lini-ulifaradhishwa-mwezi-wa-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket