Swali: Nilikuwa nimefunga na nikalala msikitini. Baada ya kuamka nikajiona kuwa nimeota. Je, kuota kunaathiri funga ya mfungaji pamoja na kuzingatia kwamba sikuoga na nikaswali pasi na kuoga. Mara nyingine nilipatwa na jiwe kichwani ambapo nikavuja damu. Je, nifungue kwa sababu ya damu? Aidha kutapika kunaharibu swawm?
Jibu: Kumwaga hakuharibu funga. Mja hakufanya kwa kutaka kwake mwenyewe. Lakini analazimika kuoga josho la janaba akitokwa na manii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa juu ya hilo akajibu kwamba ni lazima kwa ambaye ameota kuoga pale atakapoona manii.
Kitendo cha wewe kuswali bila ya kuoga ni kosa na maovu makubwa. Ni lazima kwako kurudi kuswali pamoja na kumwomba Allaah (Subhaanah) msamaha.
Jiwe lililokupata kichwani mwako mpaka ukavuja damu hakuharibu funga yako.
Matapishi yaliyokutoka pasi na kutaka kwako hakuharibu funga yako. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ambaye yatamshinda matapishi basi halazimiki kulipa. Na mwenye kujitapikisha basi ni lazima kwake kulipa.”
Ameipokea Ahmad na watunzi wa ”Sunan” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 04-05
- Imechapishwa: 29/03/2021
Swali: Nilikuwa nimefunga na nikalala msikitini. Baada ya kuamka nikajiona kuwa nimeota. Je, kuota kunaathiri funga ya mfungaji pamoja na kuzingatia kwamba sikuoga na nikaswali pasi na kuoga. Mara nyingine nilipatwa na jiwe kichwani ambapo nikavuja damu. Je, nifungue kwa sababu ya damu? Aidha kutapika kunaharibu swawm?
Jibu: Kumwaga hakuharibu funga. Mja hakufanya kwa kutaka kwake mwenyewe. Lakini analazimika kuoga josho la janaba akitokwa na manii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa juu ya hilo akajibu kwamba ni lazima kwa ambaye ameota kuoga pale atakapoona manii.
Kitendo cha wewe kuswali bila ya kuoga ni kosa na maovu makubwa. Ni lazima kwako kurudi kuswali pamoja na kumwomba Allaah (Subhaanah) msamaha.
Jiwe lililokupata kichwani mwako mpaka ukavuja damu hakuharibu funga yako.
Matapishi yaliyokutoka pasi na kutaka kwako hakuharibu funga yako. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ambaye yatamshinda matapishi basi halazimiki kulipa. Na mwenye kujitapikisha basi ni lazima kwake kulipa.”
Ameipokea Ahmad na watunzi wa ”Sunan” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 04-05
Imechapishwa: 29/03/2021
https://firqatunnajia.com/02-mfungaji-kutokwa-na-manii-na-kutapika/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)