02. Hadiyth “Sehemu kubwa ya adhabu ndani ya kaburi inatokana na mkojo… “

158 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sehemu kubwa ya adhabu ndani ya kaburi inatokana na mkojo. Hivyo basi jichungeni na mkojo!”[1]

Ameipokea al-Bazzaar, at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr”, al-Haakim na ad-Daaraqutwniy kupitia kwa Abu Yahyaa al-Qattaat, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ´Abbaas. ad-Daaraqutwniy amesema:

“Cheni ya wapokezi wake haina neno.”

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/177)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy