139- Mu´aadh bin Jabal ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mimi namdhamini nyumba kando ya Pepo, nyumba katikati ya Pepo na Pepo juu ya Pepo, kwa yule anayeacha mizozo ijapokuwa yuko na haki, akaacha kusema uongo ijapokuwa ni kwa mzaha na akaipamba tabia yake.”[1]
Ameipokea al-Bazzaar na at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam” zao tatu. Kwenye mlolongo wa wapokezi yuko Suwayd bin Ibraahiym Abu Haatim[2].
[1] Nzuri kupitia zengine.
[2] Hili ni kosa, kwa sababu Suwayd huyu hakutajwa katika Hadiyth hii. Ametajwa katika upokezi mwingine kutoka kwa Ibn ´Abbaas.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/168-169)
- Imechapishwa: 07/05/2020
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)