01. Vitabu ambavyo mwanafunzi anapaswa kuanza navyo katika ´Aqiydh

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

MAELEZO

Himdi zote njema astahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake na wale wataowapenda na kufuata mwongozo wao.

Amma ba´d:

Kitabu hiki kwa jina ”Thalaathat-ul-Usuwl” ni miongoni mwa vitabu bora katika ´Aqiydah ya wailsamu wote kwa ujumla na khaswa kwa mwanafunzi. Yule mwanafunzi anayeanza anakihitajia na yule ambaye ameshabobea katika elimu. Hiyo ina maana kwamba hakuna mwanafunzi wala muislamu yeyote anayejitosheleza nacho. Kwa hiyo kina haki zaidi kuhifadhiwa na kuelewa maana yake. Vilevile kina haki zaidi kwa waalimu na walezi – na khaswa katika yale masuala ya ´Aqiydah – kuanza kwacho katika kujifunza ´Aqiydah ya Kiislamu kabla ya kitabu chengine chochote. Kisha baada ya hapo mtu aende katika “al-Qawaa´id al-Arba´ah”, “Kashf-ush-Shubuhaat” na “Kitaab-ut-Tawhiyd”[1]. Baada ya hapo aende katika “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah”, “al-Hamawiyyah”, “at-Tadmuriyyah[2] na  “at-Twahaawiyyah”[3]. Baada ya hapo aende katika vitabu vya Sunnah ambavyo viko ndani ya vitabu vya Sunan au vitabu vya Sunnah vilivyoandikwa kando. Vitabu hivi – Allaah akitaka – yule atayemaliza maisha yake katika hali ya kutafuta elimu atavikuta vitabu hivi viko mbele yake.

[1] Mwandishi wavyo ni Imaam Mujaddid Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah).

[2] Mwandishi wavyo ni Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

[3] Cha Imaam Abu Ja´far Ahmad bin Muhammad at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twariyqal-Usuwl ilaa idhwaah-ith-Thalaat-il-Usuwl, uk. 14
  • Imechapishwa: 17/11/2021