Swali 1: Ni kwa mambo gani inapatikana kufuru kubwa au kuritadi kukubwa? Je, ni maalumu kwa kuamini, kukanusha na kukadhibisha tu au ni jambo pana zaidi ya hivo?
Jivu: Hakika kufuru na kuritadi kunapatikana kwa mambo mengi:
1 – Kukanusha jambo linalojulikana vyema katika dini.
2 – Kutenda kitendo cha kufuru.
3 – Kutamka neno la kufuru.
4 – Kwa kuacha na kuipuuza dini ya Allaah.
Kufuru inakuwa kwa kuamini. Mfano wa hilo mtu akaamini kuwa Allaah ana mke au mtoto, akaamini kuwa Allaah ana mshirika katika utawala, kwamba kuna mwingine anayesimamia uendeshaji wa ulimwengu huu pamoja na Allaah, akaamini kuwa kuna yeyote anayeshiriki na Allaah katika majina Yake, sifa Zake au matendo Yake, akaamini kuwa kuna yeyote anayestahiki kuabudiwa kinyume na Allaah au akaamini kuwa Allaah ana mshirika katika matendo Yake. Mtu anayekuwa na imani hii, anakuwa kafiri kufuru kubwa inayomtoa katika Uislamu.
Kufuru inakuwa kwa kitendo. Mfano wa hilo mtu akasujudia sanamu, akafanya uchawi, akafanya aina yoyote ya ushirikina kama vile kumwomba mwingine asiyekuwa Allaah, akachinja kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Allaah, akaweka nadhiri kwa mwingine asiyekuwa Allaah au akafanya Twawaaf katika Nyumba nyingine kinyume na Ka´bah hali ya kujikurubisha kwa kitu hicho. Kwa hiyo kufuru inakuwa kwa kitendo kama inavyokuwa kwa maneno.
Kufuru inakuwa kwa maneno. Mfano wa hilo ni mtu kumtukana Allaah, akamtukana Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akaitukana dini ya Uislamu, akafanya mzaha kwa Allaah, Qur-aan au Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kwa dini Yake. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu watu waliokuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika vita vya Tabuuk waliomfanyia mzaha yeye na Maswahabah wake:
قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ
“Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[1]
Allaah amewahukumu kuwa wamekufuru baada ya kuamini, jambo linalijulisha kuwa kufuru inakuwa kwa kitendo kama inavyokuwa kwa imani na vilevile kwa maneno, kama ilivyoelezwa katika Aayah hiyo kwamba watu hao wamekufuru kwa maneno.
Kufuru inakuwa kwa ukanushaji na imani. Mawili hayo mawili ni kitu kimoja, ingawa kunaweza kuwa na tofauti baina yao. Ukanushaji ni kama mtu akikanusha jambo ambalo linajulikana vyema katika dini. Mfano wa hilo ni mtu akakanusha uola wa Allaah, akakanusha ´ibaadah ya Allaah, kwamba Allaah pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa, akakanusha uwepo wa Malaika fulani, akamkanusha Mtume fulani, Kitabu chochote kilichoteremshwa, akakanusha kufufuliwa, Pepo, Moto, malipo, hesabu, akakanusha wajibu wa swalah, zakaah, hijjah, swawm au akakanusha wajibu wa kuwafanyia wema wazazi, wajibu wa kuunga udugu au jambo lolote linalojulikana vyema katika dini kuwa ni wajibu. Mfano mwingine akakanusha uharamu wa zinaa, riba, unywaji wa pombe, utovu wa nidhamu kwa wazazi, kukata udugu, rushwa au jambo lolote linalojulikana vyema katika dini kuwa ni haramu.
Kufuru inakuwa kwa kuipuuza dini ya Allaah, kuiacha na kuikataa. Mfano wa hilo ni mtu akaikataa dini ya Allaah kwa namna ya kujitenga nayo, asijifunze wala asimwabudu Allaah. Anakuwa kafiri kwa upuuzaji na ukataaji huu. Allaah amesema:
وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنذِرُوا مُعْرِضُونَ
“Na wale waliokufuru kwa yale wanayoonywa kwayo ni wenye kukengeuka.”[2]
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ
“Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayah za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi tutawalipiza wahalifu.”[3]
Kwa hivyo kufuru inakuwa kwa imani, kukanusha, kitendo, maneno, upuuzaji, kuacha na kukataa.
Ambaye ametenzwa nguvu kusema neno la kufuru au kutenda kitendo cha kufuru, basi anakuwa na udhuru ikiwa kulazimishwa kwake kulikuwa ni kwa nguvu kubwa. Mfano wa hilo ni mtu akilazimishwa na mwingine anayeweza kumtishia kwa kumuua au kumuweka chini ya tishio la kifo – na kweli ni muweza wa kufanya hivo – basi anakuwa na udhuru katika hali hii ikiwa atafanya kitendo cha kufuru au kutamka neno la kufuru, kwa sharti kuwa moyo wake uko tulivu juu ya imani. Hata hivyo ikiwa moyo wake umetulizana juu ya ukafiri, basi anakufuri hata kama ametenzwa nguvu. Kwa hiyo kuna aina tano ya ambaye anafanya kufuru:
1 – Akafanya kufuru kwa kumaanisha kweli, anakufuru.
2 – Akafanya kufuru kwa mzaha, anakufuru.
3 – Akifanya kufuru kwa khofu, anakufuru.
4 – Akifanya kufuru kwa kulazimishwa na wakati huohuo moyo wake umetulizana juu ya ukafiri, anakufuru.
5 – Akifanya kufuru kwa kulazimishwa na wakati huohuo moyo wake umetulizana juu ya imani, hakufuru. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِين
”Atakayemkufuru Allaah baada ya kuamini kwake [atachukuliwa hatua] – isipokuwa yule aliyelazimishwa na huku moyo wake ukawa umetua juu ya imani. Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao watapata ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kubwa. Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah na kwamba Allaah hawaongoi watu makafiri.”[4]
[1] 09:65-66
[2] 46:03
[3] 32:22
[4] 16:106
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 02-06
- Imechapishwa: 31/12/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 02-06
Imechapishwa: 31/12/2025
https://firqatunnajia.com/01-ni-kwa-mambo-gani-inapatikana-kufuru-kubwa-au-kuritadi-kukubwa/