01. Namna ilivyoandikwa ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth”

Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Mwisho mwema ni kwa wale wenye kumch Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote watukufu.

Mimi wakati nilipotoka Twabaristaan na Gilaan ili kuelekea katika nyumba tukufu ya Allaah na kutembelea kaburi la Mtume Wake Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), waliniomba ndugu zangu katika dini kuwakusanyia baadhi ya vipengele vya misingi ya dini ambavyo walishikamana barabara navyo wale maimamu walitoangulia, wanazuoni wa waislamu na Salaf wema; misingi ya dini ambayo waliongozwa kwayo, wakawalingania watu kwayo, wakawaita watu kwayo katika nyakati zote, kukemea kutokana na yale yote yanayopingna na kwenda kinyume na madhehebu ya waumini, wenye kusadikisha na wenye kumcha Allaah, wakapenda na kuchukia kwa ajili yake, wakamtia kwenye uzushi na kumkufurisha yule mwenye kuonelea kinyume chake, wakawa nayo juu ya nafsi zao wenyewe na kwa wale waliowalingania – kutokana na baraka na kheri zake na baadaye wakafurahia zile thawabu za kulazimiana na ´Aqiydah yao na kushikamana nayo barabara na kuwaelekeza waja kwayo. Hivyo nikaswali ili kumuomba Allaah (Ta´ala) ushauri na kuandika katika kijitabu hiki kwa njia fupi hali ya kutaraji wale wenye busara na wenye umaizi wataweza kunufaika nacho. Namuomba Allaah ahakikishe dhana yangu na kwa ukarimu na fadhilah Zake atutunuku tawfiyq na kunyooka sawasawa juu ya njia ya sawa na ya haki.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 9
  • Imechapishwa: 29/11/2023