Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti za swalah

MAELEZO

Masharti ni wingi wa sharti. Sharti ni kile ambacho kutokuwepo kwake kunapelekea kutokuwepo kwa jambo, lakini kuwepo kwake hakumaanishi lazima jambo litokee. Maana yake ni kwamba mtu anapokuwa hana twahara basi inampelekea kutosihi kwa swalah yake, kwa sababu miongoni mwa sharti za swalah ni kuwa na twahara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hakubali swalah ya mmoja wenu anapokuwa na hadathi mpaka atawadhe.”

al-Bukhaariy (6954) na Muslim (537) kupitia kwa Abu Hurayrah.

Mtu anaweza kutawadha kisha akapata hadathi bila kuswali swalah yoyote kwa wudhuu´ huo. Hivyo haimaanishi kwamba kuwepo kwa twahara lazima kuwe na swalah.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 4-5
  • Imechapishwa: 30/04/2026