Katika kumuamini Allaah (Subhaanah) ni kuamini kuwa Allaah ndiye mungu wa haki anayestahiki ´ibaadah pasi na vyengine vyote. Hilo ni kwa sababu Yeye ndiye muumbaji wa viumbe, mwenye kuwatendea wema, mwenye kusimamia riziki zao na anayejua ya siri yao na yale wanayoyafanya hadharani. Yeye ndiye muweza wa kumlipa mtiifu katika wao na kumuadhibu mtenda dhambi katika wao. Allaah amewaumba majini na watu kwa ajili ya ´ibaadah hii na akawamrisha nayo. Amesema (Ta´ala):

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ

“Sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu. Sitaki kutoka kwao riziki yoyote na wala sitaki wanilishe. Hakika Allaah ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, madhubuti.” (51:56-58)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambae amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kucha; ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji [na] akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi, msimfanyie Allaah washirika na hali ya kuwa nyinyi mnajua.” (02:21-22)

Allaah aliwatuma Mitume na akateremsha vitabu kwa ajili ya kubainisha haki hii na kulingania kwayo na wakati huohuo kutahadharisha yale yenye kupingana nayo. Amesema (Subhaanah):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuut [miungu ya uongo].”” (16:36)

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mungu wa haki isipokuwa Mimi – basi niabuduni!”” (21:25)

كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ

“Hichi ni Kitabu ambacho Aayah Zake zimetimizwa barabara kisha zikapambanuliwa vizuri kutoka kwa Mwenye hekima, Mjuzi wa yote; ili msiabudu yeyote isipokuwa Allaah. Hakika mimi ni muonyaji kwenu na mbashiriaji.” (11:01-02)

Uhakika wa ´ibaadah hii ni kumpwekesha Allaah (Subhaanah) katika yale yote ambayo waja wanaabudu kwayo katika du´aa, khofu, kutaraji, swalah, swawm, kuchinja, kuweka nadhiri na aina nyenginezo za ´ibaadah. Mtu anatakiwa kufanya yote hayo kwa njia ya kumnyenyekea, kuwa na shauku, kumwogopa na wakati huohuo kuwa na mapenzi kamilifu Kwake (Subaanah) na kumdhalilikia kwa sababu ya ukubwa Wake. Sehemu kubwa ya Qur-aan tukufu imeteremka juu ya msingi huu mkubwa. Amesema (Subhaanah):

فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

“Mwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini! Tanabahi, ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika.” (39:02-03)

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

“Mola wako ameamrisha, kwamba asiabudiwe yeyote isipokuwa Yeye pekee.” (17:23)

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

“Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini japokuwa wanachukia makafiri.” (40:14)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haki ya Allaah juu ya waja wamuabudu Yeye na wala wasimshirikishe na chochote.”[1]

[1] al-Bukhaariy (2701), Muslim (30), at-Tirmidhiy (2643), Ibn Maajah (4296) na Ahmad (05/238).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 05
  • Imechapishwa: 30/05/2023