1 – Kumcha Allaah. Nakuusia kumcha Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika siri na dhahiri. Huo ndio wasia wa Allaah kwa wale watu wa mwanzo na waliokuja baadaye. Amesema (Ta´ala):

وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ

”Hakika Tumewausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu na nanyi [pia tunakuusieni] kwamba: “Mcheni Allaah.”[1]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ

“Enyi walioamini! Mcheni Allaah ukweli wa kumcha.”[2]

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا

“Na yeyote yuleanayemcha Allaah, atamjaalia njia [ya kutoka katika matatizo].”[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mcheni Allaah popote unapokuwa.”[4]

Kumcha Allaah ndio wasia wa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa waja Wake na ndio wasia wa Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ummah wake. Kwa hivyo, ee dada wa Kiislamu, ni mwenye kufanyia kazi wasia huo? Namuomba Allaah (´Azza wa Jall) anifanye mimi, wewe na waislamu wote kuwa katika wachaji Allaah.

[1] 04:131

[2] 03:102

[3] 65:02-03

[4] Ahmad, at-Tirmidhiy na wengineo. Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy. Tazama ”Swahiyh-ul-Jaamiy´ as-Swaghiyr” (01/81) nr 97.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 09-10
  • Imechapishwa: 27/01/2026