01. Hadiyth “Yule mwenye kumfuturisha mfungaji… “

1078- Zayd bin al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kumfuturisha mfungaji basi anapata mfano wa ujira wake pasi na kupungua chochote katika zile thawabu za mfungaji.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” zao. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

Katika upokezi wa Ibn Khuzaymah na an-Nasaa´iy imekuja:

“Yule mwenye kumwandaa mpambanaji au akamwandaa mwenye kuhiji au akambakilia kumwangalilia familia yake au akamfuturisha mfungaji basi anapata mfano wa thawabu zake pasi na kupungua chochote katika thawabu zao.”[2]

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/623)
  • Imechapishwa: 24/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy