01. Hadiyth “Watu wawili wenye kukidhi haja wasinong´onezane… “

155 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhum) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu wawili wenye kukidhi haja wasinong´onezane[1] ambapo kila mmoja akatazama uchi wa mwenzie. Allaah huchukia jambo hilo.”[2]

Ameipokea Abu Daawuud, Ibn Maajah na tamko ni lake na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Tamko la mwisho ni kama la Abu Daawuud ambapo Abu Sa´iyd al-Khudriy amesimulia kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Watu wawili wasizungumze pindi wanapokidhi haja nje hali ya kuwa wameacha wazi nyuchi zao. Allaah huchukia jambo hilo.”

[1] Makanusho haya ni yenye maana ya makatazo.

[2] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/175)
  • Imechapishwa: 30/03/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy